Huduma ya maombi na maombezi imewekwa kwa lengo la kushirikiana na watu wenye mahitaji mbalimbali ili kumwomba Mungu kwa ajili […]
Huduma hii ya neno la Mungu inalenga kufundisha neno kupitia vitabu mbalimbali, Makala na machapisho ambayo yametafsiri neno la Mungu […]
Huduma hii inalenga kuongeza uelewa wa neno la Mungu kwa njia ya kuuliza maswali kwenye tovuti hii na kisha kupatiwa […]
Nguvu ya sadaka ni tovuti ambayo imeanzishwa mnano tarehe 01 October 2022 mahsusi kwa ajili ya kufundisha na hatimaye kufunua uelewa wa watu juu ya neno la Mungu. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe anaongea na wanadamu kupitia neno lake. Katika Yohana Mtakatifu 17:17; Yesu Kristo anasema habari ya kutakaswa katika kweli na hiyo kweli ni neno la Mungu. Kwa kutambua kuwa kweli inapatikana katika neno, nimeona ni vyema kuanzisha mahali ambapo watu watakuja na kuijua kweli kupitia tafsiri mbalimbali za neno la Mungu.
Jina la nguvu ya sadaka linatokana na ukweli kwamba ipo nguvu kubwa ya kiroho ndani ya sadaka tunazotoa mbele za Mungu lakini watu wengi pengine hawajui jambo hilo. Kwa hiyo, kupitia tovuti hii tutaeleza kwa upana sana juu ya sadaka na hatimaye kwa msaada wa nguvu za Roho Mtakatifu ninaamini watu watapona. Katika kuongeza uelewa wa kujua sadaka, nimeandika kitabu kiitwacho “Nguvu Iliyopo katika Sadaka Isiyo ya Kawaida”. Kitabu hiki kinapatika kwa mfumo wa nakala ngumu na laini kwenye tovuti hii. Kwa hiyo, ili kuongeza uelewa nitakuwa natoa ufafanuzi wa mada zote zilizo ndani ya hicho kitabu kwa njia ya sauti na picha.