Kuhusu Sisi

Nguvu ya sadaka ni tovuti ambayo imeanzishwa mnano tarehe 01 October 2022 mahsusi kwa ajili ya kufundisha na hatimaye kufunua uelewa wa watu juu ya neno la Mungu. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe anaongea na wanadamu kupitia neno lake. Katika Yohana Mtakatifu 17:17; Yesu Kristo anasema habari ya kutakaswa katika kweli na hiyo kweli ni neno la Mungu. Kwa kutambua kuwa kweli inapatikana katika neno, nimeona ni vyema kuanzisha mahali ambapo watu watakuja na kuijua kweli kupitia tafsiri mbalimbali za neno la Mungu.

Jina la nguvu ya sadaka linatokana na ukweli kwamba ipo nguvu kubwa ya kiroho ndani ya sadaka tunazotoa mbele za Mungu lakini watu wengi pengine hawajui jambo hilo. Kwa hiyo, kupitia tovuti hii tutaeleza kwa upana sana juu ya sadaka na hatimaye kwa msaada wa nguvu za Roho Mtakatifu ninaamini watu watapona. Katika kuongeza uelewa wa kujua sadaka, nimeandika kitabu kiitwacho “Nguvu Iliyopo katika Sadaka Isiyo ya Kawaida”. Kitabu hiki kinapatika kwa mfumo wa nakala ngumu na laini kwenye tovuti hii. Kwa hiyo, ili kuongeza uelewa nitakuwa natoa ufafanuzi wa mada zote zilizo ndani ya hicho kitabu kwa njia ya sauti na picha.

  1. Mbali na sadaka, kupitia tovuti hii tutafundisha neno la Mungu kwa njia ya:
    Tafsiri ya neno; tutaandika tafsiri mbalimbali za neno la Mungu katika Biblia kwa njia ya vitabu, machapisho mbalimbali, Makala na mijadala yenye lengo la kuongeza uelewa juu ya neno la Mungu.
  2. Video; kwa njia ya video, watumishi mbalimbali wa Mungu watanakili kwa njia ya sauti na picha tafsiri za maandiko matakatifu. Ujumbe wa sauti na picha utatumwa kwenye akaunti yetu ya YouTube na linki yake itakuwa hapa kwenye tovuti hii ili kurahisisha uelewa wa wasomaji wetu katika kulijua neno la Mungu.
  3. Uimbaji; nyimbo mbalimbali zilizobeba ujumbe wa neno la Mungu pia zitawekwa kwenye YouTube yetu na linki yake itapatikana hapa.
  4. Maswali na majibu; ili kupanua mjadala wa uelewa wa neno la Mungu, kupitia tovuti hii tutakuwa na ukurasa wa maswali na majibu ambapo muuliza swali ataandika swali lake kisha litapatiwa majibu.