Huduma hii inalenga kuongeza uelewa wa neno la Mungu kwa njia ya kuuliza maswali kwenye tovuti hii na kisha kupatiwa majibu kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Mungu. Watumishi wa Mungu watajibu kwa njia ya kuandika au kukupigia simu au kwa kunakili sauti na kuiweka kwenye You Tube yetu yenye jina la “Nguvu Ya Sadaka”. Mbali na kuuliza maswali kwenye tovuti hii, pia unakaribishwa kuhudhuria madarasa ya neno la Mungu katika ibada zetu. Mafundisho hayo hufanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa 10 jioni na siku ya Jumapili kwenye madarasa ya shule ya uanafunzi na maandiko.
Kwa mawasiliano juu ya huduma hii, kwa mkoa wa Dar es Salaam wasiliana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) Kimara Kilungule, Mchungaji Kundael Matee kwa namba ya simu 0655914141 au Mwalimu Mbogo Kerenge kwa namba ya simu 0763547281. Kwa mkoa wa Arusha wasiliana na Mchungaji Jonathani Kalulu wa T.A.G SEKEI PARADISE TEMPLE kupitia namba ya simu 0768818301.