Maombezi

Huduma ya maombi na maombezi imewekwa kwa lengo la kushirikiana na watu wenye mahitaji mbalimbali ili kumwomba Mungu kwa ajili ya kuleta majibu ambayo hayawezekani kwa akili za kibinadamu. Tunaamini kuwa ipo nguvu katika maombi ya watu wawili na zaidi kuliko ya mtu mmoja. Maandiko matakatifu yanasema “….kwamba wawili wenu wakipatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni(Mathayo 18:19). Hivyo kupitia huduma hii ya maombi tunaunganisha imani zetu ili kumwita Mungu juu ya mahitaji yetu maana yeye ameahidi tutakapokuwa wawili watatu yeye yupo kati yetu na atafanya.

 

Huduma ya maombi inapatikana kanisani kwetu siku ya Ijumaa ya kila wiki kuanzia saa 10 jioni. Siku ya ijumaa huwa ni maalumu kwa maombi tu. Hata hivyo huduma hii hupatikana katika siku zote za ibada kama vile ibada ya Jumatano kuanzia saa 10 jioni na siku ya Jumapili katika ibada zote mbili.

Kwa mawasiliano juu ya huduma hii, kwa mkoa wa Dar es Salaam wasiliana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) Kimara Kilungule, Mchungaji Kundael Matee kwa namba ya simu 0655914141. Kwa mkoa wa Arusha wasiliana na Mchungaji Jonathani Kalulu wa T.A.G SEKEI PARADISE TEMPLE kupitia namba ya simu 0768818301 ambaye pia anatoa huduma ya maombi kwa njia ya simu kwa siku za Jumanne, Alhamis na Ijumaa kuanzia muda wa saa 4 Asubuhi mpaka saa 10 Jioni.